AY aukwaa ubalozi

12:29 PM Posted by Unknown

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya (bongofleva) hapa nchini Ambwene Yesaya a.k.a Ay hivi karibuni ameukwaa ubalozi wa kinywaji cha Malta Guines Afrika Mashariki


Msanii huyo ambaye kiukweli ni mtaratibu na asiye na makuu,ambapo kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya uitwao Leo ataungana na mabalozi wengine waliochaguliwa kutoka Kenya kwa minajili ya kuitangaza mojawapo ya bidhaa za East afrika Breweries-Malta Guiness....


Ili kudhihirisha hilo,muda si mrefu ujao picha na sauti za mwanamuziki huyo zitatumiwa kwenye matangazo ya kinywaji hicho kisicholewesha na kinachoaminika kuongeza nguvu za mwili.Mbali ya Ay, kuna wasanii wengine ni pamoja na Esther Wahome ambaye ni muimbaji nyota wa nyimbo za injili nchini Kenya pamoja na aDj Adrian.

AY ni moja ya wakongwe wa muziki huu wa kizazi kipya hapa nchini,amewahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwemo wimbo wa Yule,Asubuhi,Leo na nyinginezo nyingi tu.
You can leave a response, or trackback from your own site.

0 Response to "AY aukwaa ubalozi"

Post a Comment

BLOG MBALI MBALI

BONGO FLAVA, BONGO DANCE, TAARAB, NYIMBO ZA INJILI, ZILIPENDWA AND ONLINE RADIO VISIT:

CHEAP WEB HOSTING, DOMAIN REGISTRATIONS AND MUCH MORE CONTACT: